VIAMBATANISHO MUHIMU WAKATI WA KUOMBA MKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU.
- Barua ya maombi ya Mkopo ikitaja kiasi cha fedha kinachoombwa na kikundi.
- Nakala ya katiba iliyohakikiwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mwanga.
- Nakala ya Cheti cha usajili wa kikundi kilichotolewa na Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mwanga.
- Historia fupi ya kikundi na Andiko la Mradi linaloonyesha mchanganuo wa mradi unaoombewa mkopo.
- Nakala ya Leseni ya biashara kwa miradi yenye uhitaji wa Leseni mfano duka, Uuzaji mifugo na Mama Lishe au Barua ya utambulisho kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji kwa miradi isiyohitaji Leseni kuonyesha uwepo na utambuzi wa Mradi katika eneo lake mfano kilimo,Ufugaji,Ufinyanzi na inayofanana na hiyo
- Nakala ya taarifa za akaunti ya kikundi (Bank Statement).
- Fomu ya Maombi ya Mkopo inayotolewa na Ofisi ya Maendeleo ya Jamii.
N:B. Kwa vikundi vya Vijana umri wao ni kuanzia miaka 18-35 pia waambatanishe nakala ya kitambulisho cha mpiga kura au cha Taifa (NIDA).
Viambatanisho vyote hivi vitawasilishwa Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) kwa ajili ya kujadiliwa na vikundi vilivyokidhi vigezo kupitishwa na kuandikiwa muhtasari na hatimaye nyaraka za vikundi kuwasilishwa Ofisi ya Maendeleo Jamii Wilaya.
IDADI
- Kikundi cha wanawake au vijana inatakiwa kiwe na idadi ya wanakikundi wasiopungua watano
- Kikundi cha watu wenye ulemavu, kinatakiwa kiwe idadi ya wanakikundi wasiopungua wawili.”
NB
- Mtu mwenye ulemavu atakuwa na sifa ya kupata mkopo kama kikundi cha watu wenye ulemavu endapo:
- Kamati ya Kudumu ya Fedha, Mipango na Uongozi itajiridhisha kuwa mtu huyo amekosa mtu mwingine mwenye ulemavu na sifa ya kuwa mwanakikundi wa kikundi cha watu wenye ulemavu;
- Anajishughulisha na ujasiriamali au anakusudia kuanzisha shughuli za ujasiriamali mdogo au wa kati;
- Ana akaunti ya benki iliyofunguliwa kwa jina lake kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kiujasiriamali;
- Ni raia wa Tanzania mwenye akili timamu na umri wa miaka kumi na nane na kuendelea;
- Hana ajira rasmi.
- Mtu mwenye ulemavu anayekusudia kuomba mkopo chini ya masharti ya kanuni hii atatakiwa kujaza fomu ya maombi ya mkopo itakayoambatishwa na nyaraka zifuatazo:
- Nakala ya cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo inayothibitisha kuzaliwa kwake.
- Nakala ya leseni ya biashara au kitambulisho cha ujasiriamali kilichotolewa na Serikali.
- Nakala halisi ya taarifa ya akaunti kutoka katika benki ambayo ana akaunti.
- Nakala halisi ya barua ya utambulisho kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji au Mtaa kwa kadri itakavyokuwa na Mtendaji wa Kata.
- Wazo la biashara.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Maofisa wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kupiga namba zifuatazo:-
0624-397249
0756-803364
0672-268953
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa
Last edited: