PISHI NA DONDOO ZA JIKONI
Pilau tulilila na kachumbari na ndizi mbivu. Share kwenye comments jinsi unavyopika pilau, viungo unavyo weka na jinsi unavyo pika. Pia ukiwa na maswali na mengineyo share kwenye comments, usisahau ku-subscribe na kushare recipe hii na uwapendao.
-Pilau ni menu mojawapo pendwa nyumbani, kwangu. Huwa napenda kupika hasa weekend, sikukuu au nikipata wageni wapenda pilau. Kulipika ni simple sio pishi complicated kama wengi wanavyo dhani, ukipika mara kwa mara utalimudu.

-Hapa nitakupa recipe yangu ya #pilaung’ombe, super simple kama unahitaji kujifunza ni bidii yk tu kufanya mazoezi ya kupika.
-Mahitaji
.mchele kilo 1
.nyama 750 gram
.vitunguu maji 3
.vitunguu saumu vikubwa 2
.mafuta kikombe kidogo 1
.viazi vikubwa 5(gawa mara 2)
-chumvi vijiko vidogo 3
-pilau msala
-tangawizi kijiko kidogo 1
-maji moto lita moja na nusu
-Mahitaji
.mchele kilo 1
.nyama 750 gram
.vitunguu maji 3
.vitunguu saumu vikubwa 2
.mafuta kikombe kidogo 1
.viazi vikubwa 5(gawa mara 2)
-chumvi vijiko vidogo 3
-pilau msala
-tangawizi kijiko kidogo 1
-maji moto lita moja na nusu

.Anza kuaandaa kila kitu osha nyama katakata, chambua osha na uache uchuje maji, menya viazi osha na andaa vitu vyote vilivyo baki.
Jinsi ya kupika
1-Nilichemsha nyama na kuweka tangawizi na chumvi kijiko kimoja, ilipo iva nikaiweka pembeni.
Jinsi ya kupika
1-Nilichemsha nyama na kuweka tangawizi na chumvi kijiko kimoja, ilipo iva nikaiweka pembeni.

2.Nikaweka jikoni sufuria ya pilau na kutia mafuta, yalipo pata moto nikatia vitunguu na kikaanga hadi vikawa brown nikatia nyama, nikaiacha kidogo kisha nikaweka vitunguu saumu nika viacha kidogo hadi vilipo anza kutoa harufu nikaweka pilau masala kisha nikamix na mwiko kuhakikisha kila kitu kimechanganyika vizuri.

-Nikatia maji, viazi, mchele na chumvi nika mix tena na mwiko k kisha nikafunika na mfuniko na kuacha pilau lichamke na kuendelea kuiva.

Maji yalipo karibia kukauka nikazima jiko na kuweka pilau ktk oven liendelee kukauka taratibu hadi lilopo kuwa tayari.

Pilau tulilila na kachumbari na ndizi mbivu. Share kwenye comments jinsi unavyopika pilau, viungo unavyo weka na jinsi unavyo pika. Pia ukiwa na maswali na mengineyo share kwenye comments, usisahau ku-subscribe na kushare recipe hii na uwapendao.