MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa utakaofanyika Aprili 2, 2025, katika viwanja vya Shirika la Elimu Tumbi, Kibaha, mkoani Pwani.
Taarifa hiyo imetolewa Machi 26, 2025, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha.
Kikwete amesema kuwa Dk. Mpango atawakabidhi vijana sita walioteuliwa kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, ambao wataongoza mbio hizo za Mwenge wa Uhuru katika mikoa yote ya nchi.
"Ninayo furaha kuwajulisha wananchi kuwa Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa utakaofanyika Aprili 2, 2025, katika viwanja vya Shirika la Elimu Tumbi, Kibaha, mkoani Pwani," amesema Kikwete.
Kwa mujibu wa Kikwete, mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu zitahusisha mikoa 31 na halmashauri 195, ambapo kwa siku 195 Mwenge huo utahamasisha amani, mshikamano, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa Watanzania wote.
Amesema kuwa Mwenge wa Uhuru mwaka huu unabeba kaulimbiu inayosema: "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu," ujumbe unaolenga kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo kwa njia ya amani.
Mbali na hilo, Mwenge wa Uhuru utatumika kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya kisekta na kisera katika muktadha wa kitaifa na kimataifa. Masuala hayo ni pamoja na mapambano dhidi ya Ukimwi, vita dhidi ya dawa za kulevya, kupinga vitendo vya rushwa, na kuhamasisha lishe bora kwa afya njema.
Kikwete ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Shirika la Elimu Tumbi, Kibaha, kushuhudia uzinduzi wa mbio hizo za Mwenge wa Uhuru.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani amemshukuru Waziri Kikwete kwa kutembelea eneo la uzinduzi na ameahidi kuwa maandalizi yote yatakamilika kwa wakati.