TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE

caleb

Member
1. Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana
Nilalapo nakuwaza wewe, niamkapo ni heri mama wee
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

2. Tanzania Tanzania, ninapokwenda safarini,
Kutazama maajabu, biashara nayo makazi,
Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu hakika
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

3. Tanzania Tanzania, watu wengi wanakusifu,
Siasa yako na desturi, ilituletea uhuru
Hatuwezi kusahau sisi, mambo mema ya kwetu hakika
Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.

My Take:-
Je wewe leo hii unaweza kusimama na kuimba wimbo huu, kifua mbele na ukiwa na furaha kama enzi zile? naona umaarufu wa wimbo huu umepotea, au na wenyewe ulikuwa ndani ya kakitabu ka AZIMIO LA ARUSHA.

Naomba kuwakilisha.
 
Back
Top