UTALII TANZANIA

prosper

Administrator
Staff member
Sekta ya Utalii nchini Tanzania ni moja ya sekta muhimu inayotoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi. Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya asili kama vile mandhari za kuvutia, maeneo ya kihistoria na ya kiakiolojia, hifadhi zenye wanyamapori wengi na baionuai mbalimbali, fukwe zisizochafuliwa na wingi wa utamaduni wa makabila 158. Nyanda za juu za kusini na kaskazini zina safu nyingi za milima ya kuvutia hasa yenye urefu wa kati ya mita 500 mpaka mita 1000 katika maeneo yaliyoizunguka. Mlima Kilimanjaro wenye urefu wa mita 5,895 na Meru mita 4,500 inayopatikana kaskazini mashariki mwa Tanzania ni milima iliyotokana na milipuko ya volkano miaka mingi iliyopita, yenye. Mwambao wa bahari una urefu wa zaidi ya kilomita 804 pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba (ambavyo kwa pamoja vinaunda Zanzibar) na kisiwa cha Mafia. Visiwa hivyo vina mkusanyiko wa vivutio vya asili, utamaduni, historia na akiolojia. Maliasili nyingine ni pamoja na Ziwa Viktoria, ziwa la pili kwa ukubwa duniani na chanzo cha mto Nile.
Sehemu hii inatoa taarifa kuhusu maeneo ya vivutio vya utalii ambayo wananchi wanapenda kuyatembelea yakihusisha maeneo ya hifadhi za wanyamapori, misitu ya asili, mapori ya akiba, utalii wa asili, makampuni ya utalii, jinsi ya kupanga safari kuja Tanzania, huduma za malazi, vyama vya kitalii na taarifa kuhusu safari za ndege.​
 
Back
Top