Maneno ya Kiswahili | Maneno ya Kiingereza |
---|---|
Ee Mungu twaomba uilinde Jumuiya Afrika Mashariki Tuwezeshe kuishi kwa amani Tutimize na malengo yetu. Kiitikio: Jumuiya Yetu sote tuilinde Tuwajibike tuimarike Umoja wetu ni nguzo yetu Idumu Jumuiya yetu. Uzalendo pia mshikamano Viwe msingi wa Umoja wetu Na tulinde Uhuru na Amani Mila zetu na desturi zetu. Kiitikio: Jumuiya Yetu sote tuilinde Tuwajibike tuimarike Umoja wetu ni nguzo yetu Idumu Jumuiya yetu. Viwandani na hata mashambani Tufanye kazi sote kwa makini Tujitoe kwa hali na mali Tuijenge Jumuiya bora. Kiitikio: Jumuiya Yetu sote tuilinde Tuwajibike tuimarike Umoja wetu ni nguzo yetu Idumu Jumuiya yetu. | Oh God we pray For preservation of the East African Community Enable us to live in peace May we fulfill our objectives Chorus: We should protect our community We should be committed and stand strong Our unity is our anchor Long live our community. Patriotism and togetherness Be the pillars of our unity May we guard our independence and peace Our culture and traditions. Chorus: We should protect our community We should be committed and stand strong Our unity is our anchor Long live our community. In industries and in farms We should work together We should work hard We should build a better community. Chorus: We should protect our community We should be committed and stand strong Our unity is our anchor Long live our community. |