Ahmed afunguka A-Z Faida za Simba Wese

prosper

Administrator
Staff member
Gm4AW45aQAARkM8-1024x682.jpeg

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amewasisitiza Wanachama wa Klabu wanaomiliki vyombo vya moto kuweka mafuta katika vituo vya Lake Energies kwakuwa kila lita moja wanayojaza klabu inapata asilimia ya mapato.

Ahmed amesema kwenye vituo vyote vya Lake Energies ukijaza mafuta kwa njia ya mtandao (simu za mkononi na Sim Banking) ambayo itakuwa inasaidia Moja kwa Moja klabu.

Tazama video hii hadi mwisho Ahmed ametaja sababu ya klabu kuingia makubaliano na Lake Energies na sio Kampuni nyingine.
 
Wacha wee, duuuh!!! Hawa ni makolo lakini kwa hili nawapongeza
Angalau umewapongeza, huu ndio tunauita uzalendo, pale linapofanyika jambo zuri basi tunalipongeza hata kama aliyefanya ni mpinzani wa jadi
 
Back
Top