BUWASA yafikisha huduma ya maji mjini 93%

prosper

Administrator
Staff member

maji1-332x221.jpg

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) mkoani Kagera imeendelea kutekeleza miradi ya maji ambapo hadi kufikia Desemba 2024 upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa Bukoba mjini ni Asilimia 93.

Mamlaka hiyo imepanua huduma zake katika baadhi ya miji midogo mkoani humo ya Muleba, Kayanga, Mtukula, Kyaka na Bunazi na kuongeza upatikanaji wa maji katika miji hiyo kutoka asilimia 78 hadi 84 kufikia Desemba 2024.


maji2.jpg




Advertisement


Kaimu meneja wa BUWASA Deogratias Sese amesema mamlaka hiyo inaendelea na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji 11 yenye thamani ya shilingi Bilioni 18.9 kati ya hiyo miradi 9 ni ya maji na miradi miwili ni ya usafi wa mazingira na maji taka.

Amesema tangu mwaka 2020 wateja wanaotumia huduma ya maji safi na mazingira wameongezeka kutoka wateja 19,500 hadi 30,149 kwa mwaka 2024 hivyo mamlaka hiyo kuongeza makusanyo kutoka shilingi Milioni 250 hadi milioni 474 kwa mwezi.


maji3.jpg



“Kwa sasa mjini huduma ya kupata maji ni masaa 24 zamani ilikuwa masaa 20 na miji tunayohudumia inapata maji kwa masaa 22 kipindi cha nyuma hata siku nzima ilipita bila kupata maji, tunajivunia jinsi serikali inavyoimarisha miradi ya maji katika maeneo yetu na tunavyoendelea kuwahudumia wananchi wetu,”amesema Masese.

Amesema BUWASA imeanza kutekeleza miradi ya kukabiliana na upotevu wa maji kwa kutumia shilingi bilioni 1.3 katika kata za Bakoba, Miembeni, Hamugembe na Bilele ambapo upotevu wa maji hadi Desemba 2024 ilikuwa ni asilimia 35 kutokana na uchakavu wa miundo mbinu.


maji4.jpg



Ametaja kwa sasa kuna upungufu wa maji katika ukanda wa juu ktika miji ya Muleba na Kayanga Mjini kwa baadhi ya maeneo ya Bukoba Mjini kutokana na upungufu wa maji katika vyanzo vya asili.

“Changamotoo nyingine ni baadhi ya taasisi kutokulipa madeni yao kwa wakati, gharama kubwa za kutibu maji kutokana na uchafuzi wa vyanzo, uchakavu wa miundo mbinu inayopoteza maji pamoja na shughuli za kibinadamu,” amesema.​
 
Waaaaooohh hongereni sana BUWASA. Hii ndio inayotakiwa, na wengine waige, sasa muhimu BUWASA isibweteke, Bali iendelee kuchapa kazi
 
Waaaaooohh hongereni sana BUWASA. Hii ndio inayotakiwa, na wengine waige, sasa muhimu BUWASA isibweteke, Bali iendelee kuchapa kazi
Umenena vyema, tusije tukamsifia sana mgema halafu tembo akalitia maji.
 
Back
Top