Serikali ya Rwanda imefunga rasmi Ubalozi wake nchini Ubelgiji kufuatia kukatishwa kwa uhusiano wa Kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ubalozi wa Rwanda huko Hague, Uholanzi, sasa utashughulikia huduma za kibalozi kwa Wanyarwanda wanaoishi Ubelgiji.
Licha ya kuvunjika kwa Kidiplomasia, Wizara ilifafanua kuwa raia wa Ubelgiji wanaoishi au kusafiri kwenda Rwanda hawataathirika.
Rwanda ilikata uhusiano na Ubelgiji mnamo Machi 17. Uamuzi huo uliashiria kuongezeka kwa mvutano kati ya Mataifa hayo mawili.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda ilihusisha hatua hiyo na majaribio ya kusikitisha ya Ubelgiji kuendeleza udanganyifu wake wa ukoloni mamboleo na kulishutumu taifa hilo la Ulaya kwa kuhujumu maslahi ya Rwanda, hasa katika muktadha wa mzozo unaoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).