🤪😄 ETI ANAUZA KITIMOTO NA HAJANIAMBIA😂😂

caleb

Member
Jamaa alikuwa baa anakunywa, rafiki yake akaja wakawa katika mazungumzo;

  • RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
  • JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
  • RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
  • JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
  • RAFIKI: Nini tena?
  • JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
  • RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?
  • JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, “Huyo nguruwe umeshamuondoa?’ Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja
 
Back
Top